Alhamisi, 4 Januari 2018

Umuhimu wa utafiti wa kifonetiki katika kiswahili.

 Image result for fonetiki

 

 

Umuhimu wa utafiti wa kifonetiki

 

 Image result for fonetiki

 

 


Kati ya matawi hayo matatu, Fonetiki-tamshi ndilo tawi ambalo limechunguzwa kwa undani zaidi na kwa muda mrefu sana (hasa kutokana na changamoto iliyotokana na kugundulika kwa sarufi ya Sanskrit na wanazuoni wa nchi za Ulaya Magharibi katika kame ya kumi na nane, kama tulivyosema hapo mwanzo). Istilahi nyingi za kifonetiki zinazotumiwa na wanaisimu zinahusiana na tawi hili. Katika sura hii, hili ndilo tawi ambalo tutaliangalia.
Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa katika Fonetiki-safirishi umesaidia sana katika kutia nguvu baadhi ya mahitimisho yaliyofikiwa na wataalamu wa Fonetiki-tamshi. Kwa mfano:-
i) imethibitika kuwa kila sauti inayotolewa na kiungo-sauti cha mwanadamu ni tofauti na nyingine kwa kiasi fulani. Hivyo sifa bainifu zinazotolewa kuhusu foni (kama tutakavyoona hivi punde) ni za wastani, na kuna mambo mengi ambayo yanaachwa, mambo ambayo mwanafonetiki anaona kuwa hayasaidii katika kufanikisha mawasiliano kati ya wajua-lugba. Ni wazi, kwa mfano, kuwa kuna tofauti kati ya matamshi ya mtu mwenye furaha, mwenye huzuni, mwenye mafua, au mgojwa taabani. Lakini wote bawa, ikiwa lugha wanayozungumza ni Kiswahili, wakitamka neno ‘mwanangu’ litasikika kuwa ni neno hilo hilo, yaani wote watalipa maana moja. Tofauti za matamshi zinazotokana na hali za wazungumzaji haziingizwi katika uchambuzi wa fonetiki-tamshi. Vivyo hivyo, neno rahisi la Kiswahili kama ‘kiti’ linaweza kutamkwa kwa njia tofauti na wazungumzaji tofauti au na mzungumzaji huyo huyo katika wakati na mazingira tofauti: [khiti], [kithi], au [kiti]. Matamshi ya kwanza ya neno hilo yana mpumuo katika kipasuo [k], matamshi ya pili yanaweka mpumuo katika kipasuo [t], na matamshi ya tatu hayana mpumuo popote. Katika Kiswahili Sanifu mpumuo si sifa inayotofautisha maneno, yaani si sifa bainifu. Lakini sifa hiyo hiyo ya mpumuo ni muhimu katika lugha nyingine kama vile Kihindi na Kiswahili cha Pemba (Kipemba). Kwa sababu hiyo, wanafonetiki ni lazima waonyeshe tofauti hiyo kati ya sauti.
ii) Fonetiki-safirishi imethibitisha dai la fonetiki-tamshi kuwa semi zinapotamkwa, hazikatwikatwi katika sauti moja moja kama mazoea yetu ya maandishi (na hata ya alama za IPA) yanavyotushawishi Kama vile mawimbi yanavyosafirishwa hewani, semi pia huundwa na mfululizo wa sauti. Hivyo mikato tunayoiweka kati ya sauti moja na nyingine ni ya kukadiria kwa kiasi, kikubwa. Kwa mfano, katika neno baba si rahisi kujua hasa [b] inaishia wapi na [a] inaanzia wapi. Ndiyo sababu inakuwa vigumu kutamka sauti konsonanti nyingine bila kuziwekea irabu (bila shaka unakumbuka jinsi ulivyofundishwa alfabeti shuleni!). Ni kweli pia kwamba sauti zinazofuatana katika matamsbi huathiriana sana. Hali hii huongeza ugumu wa kuziainisha.
Katika Fonetiki-tamshi, sauti zinaainishwa kufuatana na vigezo vikuu viwili:
a) Mahali zinapotamkiwa - yaani ni viungo-sauti vipi vinatumika katika utoaji wa sauti hizo.
b) Jinsi zinavyotamkwa - yaani kunatokea nini wakati hewa inatoka mapafuni kupitia kwenye ‘mrija-hewa’, kupitia kwenye glota, mpaka kufikia kwenye ‘mkondo-sauti’. Katika sehemu zifuatazo, vigezo hivi vitachunguzwa kwa undani.

Jumatano, 3 Januari 2018

JE? WAJUA KUWA FONETIKI NI MOYO WA FANOLOJIA?



Fonetiki na Fonoloji.

Fasili ya taaluma ya fonolojia haiwezi kukamilika, na pengine kueleweka iwapo hakuna linalosemwa kuhusuiana na taaluma ya fonetiki. Hali hii inatokana na ukweli kuwa kuna uhusiano wa kinasaba kati ya fonolojia na fonetiki. Massamba na wenzake (2004:5) wanaeleza ukweli huu kwamba:

Fonetiki na fonolojia ni matawi mawili tofauti ya isimu lakini yenye kuhusiana sana. Uhusiano wa matawi haya unatokana na ukweli kwamba yote mawiliyanajihusisha na uchunguzi na uchambuzi unaohusu sauti za lugha za binadamu.

Kutokana na ukweli huu, jitihada za kufasili dhana ya fonolojia inaelekea kuwa nyepesi, dhana hizi mbili zinapofasiliwa kwa mlinganyo. Tuanze na fonetiki.

Fonetikini Nini?

Fonetiki ni tawi la isimu linalochunguza sauti za kutamkwa na binadamu ambazo huweza kutumika katika lugha asilia. Massamba na wenzake (kama hapo juu) wanafasili fonetiki kuwa ni tawi la isimu linalohusika na uchunguzi na uchambuzi wa taratibu za utoaji, utamkaji, usafirishaji, usikilizaji na ufasili wa sauti za lugha za binadamu kwa ujumla. Wanasisitiza kwamba, kinachochunguzwa katika fonetiki ni (maumbo mbalimbali ya sauti zinazoweza kutolewa na alasauti za binadamu (yaani sauti za binadamu zinazotamkwa tu). Kipashio cha msingi cha uchambuzi wa kifonetiki ni foni.

Foni ni sauti yoyote inayotamkwa na binadamu na inayoweza kutumika katika lugha fulani. Hivyo basi, foni ni nyingi sana na hazina maana yoyote. Wanafonetiki hudai kuwa foni zimo katika bohari la sauti (dhana dhahania) ambalo kila lugha huchota sauti chache tu ambazo hutumika katika lugha mahususi. Sauti chache zinazoteuliwa na lugha mahususi kutoka katika bohari la sauti huitwa fonimu.

Matawi ya Fonetiki: Kuna mitazamo miwili tofauti kuhusiana na matawi ya fonetiki. Mtazamo wa kwanza ni ule unaodai kuwepo matawi matatu; na mtazamo wa pili ni ule niunaodai kuwepo matawi manne. Mtazamo wa kuwepo matawi matatu unataja fonetiki matamshi, fonetiki akustika, nafonetiki masikizi. Mtazamo wa kuwepo matawi manne. (kama Massamba na wenzake ( kama hapo juu), pamoja na matawi tuliyokwisha yataja, wanaongeza tawi fonetiki tibamatamshi.

Fonetiki mahuchunguza jinsi sauti za lugha zinavyotamkwa kwa kutumia alasauti. Hususani, huchunguza namna na mahali pa kutamkia sauti husika. Fonetiki akustika huchunguza jinsi mawimbi ya sauti yanavyosafiri kutoka katika kinywa cha mtamkaji hadi kufika katika sikio la msikilizaji. Fonetiki masikizi hujihusisha na mchakato wa ufasili wa sauti za lugha, hususani uhusiano uliopo baina ya neva za sikio na za ubongo. Na fonetiki tibamatamshi ni tawi jipya lililozuka mwanzoni mwa karne hii, ambalo huchunguza matatizo ya utamkaji ambayo binadamu huweza kuzaliwa nayo au kuyapata baada ya kuzaliwa. Ni tawi linalojaribu kutumia mbinu za kitabibu kuchunguza matatizo na namna ya kuyatatua.

Fonolojia ni Nini?

Fonolojia ni taaluma ya isimu inayochunguza mifumo ya sauti za kutamkwa zinazotumika katika lugha asilia mahususi za binadamu. Inapolinganishwa na fonetiki, inasisitizwa kuwa fonolojia ni tawi la isimu linalochunguza mifumo ya sauti za lugha mahususi tu, kama vile sauti za kiswahili, Kiingereza, Kikongo, n.k. Hata hivyo, wapo wanaisimu wanaoelekea kukubaliana kuwa kuna fonetiki ya lugha mahususi pia, na kuna fonolojia ya jumla, na fonetiki ya lugha mahususi. Mathalani, Massamba (1996) licha ya kufasili kuwa fonolojia ni taaluma ya isimu inayochunguza mfumo wa sauti za lugha mahususi, anaenda mbele zaidi na kudai kuwa fonolojia inaweza kuchunguza sauti kwa ujumla wake bila kuzihusisha na lugha mahususi.

Akmajian na wenzake (2001), nao wanadokeza msimamo kama wa massamba wanapodai kwamba fonolojia inaweza kuchunguzwa kwa mitazamo miwili tofauti. kwanza, fonolojia kama tawi dogo la isimu linalochunguza mfumo na ruwaza za sauti za lugh mahususi ya binadamu; pili fonolojia kama sehemu ya nadharia ya jumla ya lugha ya binadamu inayohusika na tabia za jumla za mfumo wa sauti za lugha asili za binadamu. Katika mhadhara huu, hata hivyo tutakuwa wafuasi wa mtazamo unaoona kuwa fonolojia ni tawi la isimu linaloshughulikia mfumo wa sauti za lugha mahususi, hivyo tuna kwa mfano, fonolojia ya Kiswahili, fonolojia ya Kiingereza, fonolojia ya Kiha, fonolojia ya Kihehe, na fonolojia ya Kibena. Kipashio cha msingi cha fonolojia ni fonimu.

Fonimu.

Ni kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia kinachoweza kubadili maana ya neno. Hivyo basi, fonimu ina maana, kwa kuwa inaweza kubadili maana ya neno inapobadilishwa nafasi katika neno husika. Foni chache zilizoteuliwa kutoka katika bohari la sauti ili zitumike kwenye mfumo wa sauti za lugha mahususi ndiyo fonimu. Hivyo, fonimu ni chache ikilinganishwa na foni. Idadi ya fonimu za lugha hutofautiana kati ya lugha moja na nyingine. Mathalani, Kiarabu kina fonimu ishirini na nane (28), Kiswahili kina fonimu thelathini (30), Kifaransa kina fonimu thelathini na tatu (33) na Kiingereza kina fonimu arobaini na nne (44). Sauti ambayo huweza kubadilishwa nafasi yake katika neno lakini maana ikabaki ileile huitwa alofoni.

Alofoni ni kishio cha kifonolojia kinachotaja hali ambapo fonimu moja hutamkwa na kuandikwa tofautitofauti bila kubadili maana ya neno. Mfano:

· Fedha na feza

· Sasa na thatha

· Heri na kheri

Kwa kifupi, alofoni ni matamshi tofautitofauti ya fonimu [sauti] moja.

Mitazamo juu ya Dhana ya Fonimu.

Juhudi za kufasili dhana ya fonimu zilizofanywa na wanaisimu mbalimbali zimezua mitazamo mbalimbali ya namna ya kuchambua dhana hii. Hadi sasa, mitazamo mitatu ifuatayo ndiyo hujulikana zaidi.

(i) Fonimu ni tukio la Kisaikolojia.

Huu ni mtazamo uliokuzwa na kutetewa na wanasarufi geuzi-zalishi, mwanzilishi wake akiwa ni Noam Chomsky. Kwa mujibu wa mtazamo huu, fonimu ni dhana iliyo katika akili ya mzungumzaji wa lugha. Mtazamo huu unadai kuwa kila mzungumzaji wa lugha ana maarifa bubu ya idadi na jinsi ya kutamka fonimu za lugha yake Chomsky anayaita maarifa haya kuwa ni umilisi (competence). Anadai kuwa maarifa haya ya fonimu hufanana kwa kiasi kikubwa miongoni mwa wazungumzaji wa lugha moja husika. Kinachotofautiana ni jinsi ya kudhihirisha (kutamka) fonimu hizo, yaani utendi (performance). Chomsky anabainisha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuhitilafiana baina ya umilisi na utendi kutokana na matatizo mbalimbali ambayo mzungumzaji hukabiliana nayo. Matatizo hayo ni kama vile uchovu, ulemavu wa viungo vya matamshi (alasauti za lugha), athari za mazingira, ulevi na maradhi. Hivyo kutoka na hali hii, fonimu hubaki kuwa tukio la kiakili, yaani kisaikolojia tu.

(ii) Fonetikinitukio la Kifonetiki.

Wafuasi wa mtazamo huu wanaongozwa na Daniel James. Ambaye anaiona fonimu kuwa ni {umbo} halisi linalojibainisha kwa sifa zake bainifu. Anadai kuwa fonimu huwakilisha umbo halisi la kifonetiki na inapotokea kukawa na fungu la sauti katika fonimu moja, sauti hizo huwa na sifa muhimu za kifonetiki zinazofanana. Hivyo, fonimu ya Kiswahili ni kitita cha sauti za msingi pamoja na alofoni zake.

(iii) Fonimu ni Fonolojia.

Huu ni mtazamo wa kidhanifu, ambapo huaminika kuwa fonimu ni kipashio cha kimfumo, yaani fonimu huwa na maana pale tuinapokuwa katika mfumo mahususi. Mwanzilishi wa mtazamo huu ni Nikolai Trubetzkoy. Yeye huamini kuwa fonimu ni dhana ya kiuamilifu na uamilifu huu hujitokeza tu fonimu husika inapokuwa katika mfumo wa sauti wa lugha husika. Kwa mujibu wa mtazamo huu, fonimu ni kipashio kinachobainisha maana ya neno. Mtazamo huu hutumia jozi sahihi kudhihirisha dai lake. Mathalani, maneno baba na bata yana maana tofauti kwa sababu ya tofauti ya fonimu /b/ na /t/. Mtazamo huu hujulikana kuwa ni wa kifonolojia. Na kwa hakika, mawazo haya ndiyo yaliyoshika mzizi zaidi katika taaluma ya fonolojia na ndiyo inayofunzwa hivi sasa katika sehemu nyingi ulimwenguni.

UhusianokatiyaFonetikinaFonolojia


FONETIKI

FONOLOJIA


HuchungasautizakutamkwanaBinadamu

HuchunguzasautizakutamkwanaBinadamu


Ni pana {huchunguzasautinyingi}

Ni finyu {huchunguzasautichachetu}


Ni kongwe.

Ni changa.


Huchunguzasautipekepeke

Huchunguzasautikatikamfumo.


Huchunguzasautikwaujumla

Huchunguzasautizalughamahususi, kama Kiswahili, naKinyeramba.


Kipashio cha msinginifoni

Kipashio cha msinginifonimu.





UhusianokatiyaFoninaFonimu.


FONI

FONIMU


Hazimamaana

Zinamaana


Zipopekepeke

Zimokatikamfumo


Nyingi

Chache





Huwezakujitokezakamaalofoni


Zinaponukuliwa, alamayamabano, “{ }” hutumika

Zinaponukuliwa, alamayamabanomshazari, “/ /” hutumika


Jumanne, 2 Januari 2018

ALA ZA SAUTI KATIKA FONETIKI YA KISWAHILI


Sauti za Kiswahili





SAUTI ZA KISWAHILI









Aina Kuu
Konsonanti





a, b, ch, d, e, f, g, h, i, k, l, m, n, o, p, r, s, t, u, v, w, y, z
Kuna aina mbili za Sauti katika lugha ya Kiswahili:

  1. Irabu
  2. Konsonanti

Irabu (Vokali)

a, e, i, o, u


Irabu zinapotamkwa, hewa haizuiliwi katika ala za matamshi.
Jedwali lifuatalo litakuonyesha jinsi ya kubainisha vokali kulingana na sehemu ya ulimi inayoachilia hewa, na jinsi midomo inavyobadilika

IrabuSehemu ya Ulimi Midomo
e,iMbele Midomo imetandazwa
a Katikati; ulimi huinuka na kutandaza Midomo imetandazwa
o,u Nyuma Midomo imevirigwa

Konsonanti

b, ch, d, f, g, h, j, k, l, m, n, p, r, s, t, v,w, y, z


Konsontanti zinapotamkwa, hewa huzuiliwa katika ala za matamshi ( ulimi na midomo).
Kuna aina mbili kuu za sauti za konsonanti:

  1. Sauti Ghuna => konsonanti hizi zinapotamkwa, hewa hutikisa nyuzi za sauti
  2. Sauti Sighuna => konsonanti hizi zinapotamkwa, hewa haitikisi nyuzi za sauti


Jedwali lifuatalo litakuonyesha aina za konsonanti kulingana na mahali zinapotamkiwa na sauti (ghuna au sighuna)


MidomoMidomo + MenoMeno + Ulimi Ufizi Kaakaa + ufizi Kaakaa gumu Kaakaa Laini Koo Aina ya Sauti
Vipasuop
d
t
d
jk
g
sighuna
ghuna
Vikwamizo / Vikwaruzof
v
th
dh
s
z
shkh
gh
hsighuna
ghuna
Kipasuo - kwamizochsighuna
Nazali / Ving'ong'omnnyng'ghuna
Kitambazal ghuna
Kimadenderghuna
Viyeyusho / Nusu Irabuywghuna



Vipasuo ( p,b,k,g,t,d )


Hutamkwa kwa kukutanisha ala za kutamkia ili kufungilia hewa na kisha kuiachilia ghafla
  • Vipasuo sighuna (p, k, t ) - hutamkwa bila kutikisa nyuzi za sauti
  • Vipasuo ghuna (b, g, d ) - hutamkwa kwa kutikisa nyuzi za sauti


/p/ na /b/ hutamkwa kwa kukutanisha midomo katika meno:
  • /p/ - papa, pepea, pipi, popo, pua
  • /b/ - baba, bebea, bibi, bobo, bubu


/t/ na /d/ hutamkwa kwa kukutanisha ufizi na ncha ya ulimi

  • /t/ - taa, tetea, titi, toto, tua
  • /d/ dada, doa, dua


/k/ na /g/ hutamkwa kwa kukutanisha nyuma ya ulimi na kaakaa laini
  • /k/ - kaka, koko, kuku
  • /g/ - gae, gege, gogo, gugu

Vikwamizo ( d f,v,dh,th, s,z,sh,h,gh)


Pia huitwa Vikwaruzo Hutamkwa kwa kukutanisha ala za matamshi na kisha kuachilia hewa kupitia katika mwanya mwembamba
  • Vikwamizo sighuna (f,th,s,kh,h,sh) - hewa haitikisi nyuzi za sauti
  • Vikwamizo ghuna (v, dh,z,gh) - hewa hutikisa nyuzi za sauti


/f/ na /v/ hutamkwa kwa kukutanisha mdomo wa chini na wa juu na kuachilia hewa kidogo kupita
  • /f/ - faa, fee, fua
  • /v/ - vaa, vua


/s/ na /z/ hutamkwa kwa kukutanisha sehemu ya kati ya ulimi na kaakaa gumu
  • /s/ - sasa, sisi
  • /z/ - zaa, zeze, zizi, zuzu


/dh/ na /th/ hutamkwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na meno ya juu
  • /dh/ - dharau, dhani
  • /th/ - thubutu


/gh/ na /kh/ hutamkwa kwa kukutanisha kaakaa laini na kilimi
  • /dh/ - dharau, dhani
  • /th/ - thubutu


/h/ hutamkwa kwa kukutanisha kilimi na koo na kuachilia hewa kwa nguvu
  • /h/ - haha, hii, huu

Kipasuo-kwamizo: ( ch )


Pia huitwa kituo-kwamizo - Hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na ufizi, na kuachilia hewa
  • /ch/ - chacha, chechea, choo

Ving'ong'o / Nazali ( m,n,ng',ny )


Hutamkwa kwa kukutanisha ala za matamshi na kuzuia hewa kupitia kinywani; hewa hupitia puani.
/m/ hutamkwa kwa kukutanisha mdomo wa juu na wa chini, ili kuzuia pumzi kupita kinywani
  • /m/ - mama, umeme, mimi,


/n/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na ufizi, ili hewa ipitie puani
  • /n/ - nana, nene, nini, nono, nunua


/ny/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na kaakaa gumu
  • /ny/ - nyanya, nyenyea, nyinyi, nyoa, nyunyu


/ng'/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na kaakaa laini
  • /ng'/ - ng'ang'a, ng'oa

Kitambaza ( l )


Hutamkwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na ufizi huku hewa ikipitia kwenye pande za ulimi bila kukwaruza ufizi
  • /l/ - lala, lea, lilia, lo! lulu

Kimadende ( r )


Hutamkwa kwa kupigapiga na kukwaruza ufizi haraka haraka kwa ncha ya ulimi.
  • /r/ - rai, rarua,

Viyeyusho ( y,w )


Pia huitwa nusu-irabu. Hutamkwa kwa utaratibu kwa kuleta ala za matamshi karibu sana lakini kuachilia hewa bila kuikwaruza.
/w/ hutamkwa midomo ikiwa wazi
  • /w/ - wawa, wewe,


/y/ hutamkiwa kwenye kaakaa gumu
  • /y/ - yaya, yeye,



Ala za Kutamkia


Hizi ni sehemu za mwili zinazotumika wakati wa kutamkia maneno:
Meno, Ulimi, Midomo, Pua, Chemba cha Pua, Ufizi, Kaakaa gumu, Kaakaa laini, Kimio , Chemba cha Kinywa, Ncha ya ulimi, Bapa la ulimi, Shina la Ulimi, Koromeo, Kidakatonge, Kongomeo, Nyuzi za Sauti, Koo, Njia ya Chakula

MAANA YA FONETIKI

               MAANA YA FONETIKI KWA MUJIBU WA WATAALAMU MBALIMBALI

Mgulu(2001-20)anasema kwa mujibu wa Hayman(19790) Fonetik ni taaluma ambayo hususan huchunguza sauti ambazo hutumiwa na binadamu . 
Habwe na Karanja(2004-20)ni taaluma ya sayansi inachunguza sauti za biaadamu . 
Image result for matawi ya fonetiki
Massamba (2007-20)Ni tawi la isimu ambalo linajishughulisha na sauti za lugha za binaadamu  .