Jumanne, 2 Januari 2018

ALA ZA SAUTI KATIKA FONETIKI YA KISWAHILI


Sauti za Kiswahili





SAUTI ZA KISWAHILI









Aina Kuu
Konsonanti





a, b, ch, d, e, f, g, h, i, k, l, m, n, o, p, r, s, t, u, v, w, y, z
Kuna aina mbili za Sauti katika lugha ya Kiswahili:

  1. Irabu
  2. Konsonanti

Irabu (Vokali)

a, e, i, o, u


Irabu zinapotamkwa, hewa haizuiliwi katika ala za matamshi.
Jedwali lifuatalo litakuonyesha jinsi ya kubainisha vokali kulingana na sehemu ya ulimi inayoachilia hewa, na jinsi midomo inavyobadilika

IrabuSehemu ya Ulimi Midomo
e,iMbele Midomo imetandazwa
a Katikati; ulimi huinuka na kutandaza Midomo imetandazwa
o,u Nyuma Midomo imevirigwa

Konsonanti

b, ch, d, f, g, h, j, k, l, m, n, p, r, s, t, v,w, y, z


Konsontanti zinapotamkwa, hewa huzuiliwa katika ala za matamshi ( ulimi na midomo).
Kuna aina mbili kuu za sauti za konsonanti:

  1. Sauti Ghuna => konsonanti hizi zinapotamkwa, hewa hutikisa nyuzi za sauti
  2. Sauti Sighuna => konsonanti hizi zinapotamkwa, hewa haitikisi nyuzi za sauti


Jedwali lifuatalo litakuonyesha aina za konsonanti kulingana na mahali zinapotamkiwa na sauti (ghuna au sighuna)


MidomoMidomo + MenoMeno + Ulimi Ufizi Kaakaa + ufizi Kaakaa gumu Kaakaa Laini Koo Aina ya Sauti
Vipasuop
d
t
d
jk
g
sighuna
ghuna
Vikwamizo / Vikwaruzof
v
th
dh
s
z
shkh
gh
hsighuna
ghuna
Kipasuo - kwamizochsighuna
Nazali / Ving'ong'omnnyng'ghuna
Kitambazal ghuna
Kimadenderghuna
Viyeyusho / Nusu Irabuywghuna



Vipasuo ( p,b,k,g,t,d )


Hutamkwa kwa kukutanisha ala za kutamkia ili kufungilia hewa na kisha kuiachilia ghafla
  • Vipasuo sighuna (p, k, t ) - hutamkwa bila kutikisa nyuzi za sauti
  • Vipasuo ghuna (b, g, d ) - hutamkwa kwa kutikisa nyuzi za sauti


/p/ na /b/ hutamkwa kwa kukutanisha midomo katika meno:
  • /p/ - papa, pepea, pipi, popo, pua
  • /b/ - baba, bebea, bibi, bobo, bubu


/t/ na /d/ hutamkwa kwa kukutanisha ufizi na ncha ya ulimi

  • /t/ - taa, tetea, titi, toto, tua
  • /d/ dada, doa, dua


/k/ na /g/ hutamkwa kwa kukutanisha nyuma ya ulimi na kaakaa laini
  • /k/ - kaka, koko, kuku
  • /g/ - gae, gege, gogo, gugu

Vikwamizo ( d f,v,dh,th, s,z,sh,h,gh)


Pia huitwa Vikwaruzo Hutamkwa kwa kukutanisha ala za matamshi na kisha kuachilia hewa kupitia katika mwanya mwembamba
  • Vikwamizo sighuna (f,th,s,kh,h,sh) - hewa haitikisi nyuzi za sauti
  • Vikwamizo ghuna (v, dh,z,gh) - hewa hutikisa nyuzi za sauti


/f/ na /v/ hutamkwa kwa kukutanisha mdomo wa chini na wa juu na kuachilia hewa kidogo kupita
  • /f/ - faa, fee, fua
  • /v/ - vaa, vua


/s/ na /z/ hutamkwa kwa kukutanisha sehemu ya kati ya ulimi na kaakaa gumu
  • /s/ - sasa, sisi
  • /z/ - zaa, zeze, zizi, zuzu


/dh/ na /th/ hutamkwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na meno ya juu
  • /dh/ - dharau, dhani
  • /th/ - thubutu


/gh/ na /kh/ hutamkwa kwa kukutanisha kaakaa laini na kilimi
  • /dh/ - dharau, dhani
  • /th/ - thubutu


/h/ hutamkwa kwa kukutanisha kilimi na koo na kuachilia hewa kwa nguvu
  • /h/ - haha, hii, huu

Kipasuo-kwamizo: ( ch )


Pia huitwa kituo-kwamizo - Hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na ufizi, na kuachilia hewa
  • /ch/ - chacha, chechea, choo

Ving'ong'o / Nazali ( m,n,ng',ny )


Hutamkwa kwa kukutanisha ala za matamshi na kuzuia hewa kupitia kinywani; hewa hupitia puani.
/m/ hutamkwa kwa kukutanisha mdomo wa juu na wa chini, ili kuzuia pumzi kupita kinywani
  • /m/ - mama, umeme, mimi,


/n/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na ufizi, ili hewa ipitie puani
  • /n/ - nana, nene, nini, nono, nunua


/ny/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na kaakaa gumu
  • /ny/ - nyanya, nyenyea, nyinyi, nyoa, nyunyu


/ng'/ hutamkwa kwa kukutanisha ulimi na kaakaa laini
  • /ng'/ - ng'ang'a, ng'oa

Kitambaza ( l )


Hutamkwa kwa kukutanisha ncha ya ulimi na ufizi huku hewa ikipitia kwenye pande za ulimi bila kukwaruza ufizi
  • /l/ - lala, lea, lilia, lo! lulu

Kimadende ( r )


Hutamkwa kwa kupigapiga na kukwaruza ufizi haraka haraka kwa ncha ya ulimi.
  • /r/ - rai, rarua,

Viyeyusho ( y,w )


Pia huitwa nusu-irabu. Hutamkwa kwa utaratibu kwa kuleta ala za matamshi karibu sana lakini kuachilia hewa bila kuikwaruza.
/w/ hutamkwa midomo ikiwa wazi
  • /w/ - wawa, wewe,


/y/ hutamkiwa kwenye kaakaa gumu
  • /y/ - yaya, yeye,



Ala za Kutamkia


Hizi ni sehemu za mwili zinazotumika wakati wa kutamkia maneno:
Meno, Ulimi, Midomo, Pua, Chemba cha Pua, Ufizi, Kaakaa gumu, Kaakaa laini, Kimio , Chemba cha Kinywa, Ncha ya ulimi, Bapa la ulimi, Shina la Ulimi, Koromeo, Kidakatonge, Kongomeo, Nyuzi za Sauti, Koo, Njia ya Chakula

Maoni 33 :

  1. je ala za kutamkia ni sawa na ala za sauti?

    JibuFuta
  2. Daaaaaa.... Safi sana, 👍👍

    JibuFuta
  3. Kiungo kinacho tetemeka na kutoa sauti huitwaje

    JibuFuta
    Majibu
    1. Mm pia nasubiria jawabu la hili swali

      Futa
  4. Ala za matamshi juu itwa aje kwa kiingereza?

    JibuFuta
  5. Asante sana kwa kuniezesha kufanya zoezi langu.Nimefahamu mengi zaidi Mungu awabariki

    JibuFuta
  6. Nimefahamu mengi mungu akubariki

    JibuFuta
  7. Kazi hii imekua ya muhimu sana kwa ufahamuzi wa utamkaji wa sauti mbali mbali na ala husika katika utoaji wa sauti kadhaa katika lugha.

    JibuFuta
  8. Ala za sauti si saut asiliaa kauli hi inamaaana gani

    JibuFuta
  9. Ni mchoro upi unaweza kuonesha ala sauti za kiswahili zinavyotamkwa?

    JibuFuta
  10. Meipenda kazi hii . MUNGU akupe maono mengine

    JibuFuta
  11. Kwa kweli mmeweza kuzichambua sauti za kiswahili kwa ubora wa Hali ya juu

    JibuFuta
  12. Kazi hii imeweza kuonyesha sauti mbalimbali kwa uzuri

    JibuFuta
  13. Umuhiwa was dhana ya sauti katika fasihi ya lugha,eleza.

    JibuFuta
  14. Linganua sautI /ch/ na /j/

    JibuFuta